Jumanne Januari 8, 2013
Tanzania House, Washington DC:
Hii ni sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano kati ya JAMII PRODUCTION na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico (anayemaliza muda wake) Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar.
Katika sehemu ya kwanza anaelezea
1: Historia ya maisha yake (kwa ufupi)
2: Ilikuwaje akaingia katika fani ya sheria? Na ni nini alipanga kufanya kabla ya kuamua kuwa mwanasheria?
3: Ni vipi alipokea ombi la kuwa Balozi?
4: Ni changamoto zipi anazokutana nazo kwenye kazi yake ya ubalozi?
5: Ni vipi anabadili mawazo ya waMarekani wanaoiona Tanzania kama nchi isiyopiga hatua?
6: Anawashirikisha vipi viongozi wa Tanzania katika maendeleo anayoyaona Marekani?
7: Ipi nafasi ya mwanamke katika uongozi?
8: Anazungumzia vipi suala la viti maalum kwa wanawake?
9: Je! Tanzania ipo tayari kuwa na Rais mwanamke? Na Je! Tanzania ina wanawake ambao wanaweza kuwa rais wa nchi?
Na mengine mengi.
KARIBU UUNGANE NASI,
Mubelwa T. Bandio wa Jamii Production