Follow by Email

Monday, February 20, 2012

Meya wa Milwaukee atangaza siku ya Tanzania, Mjini Milwaukee Wisconsin


Milwaukee, WI: Meya wa Milwaukee kwenye Jimbo la Wisconsin amemtunukia Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar hati ya kuitambua siku ya tarehe 20.02.2012 kama siku ya Tanzania mjini Milwaukee.
Mayor Thomas Barrett ametangaza siku hiyo ofisini kwake leo (jana) kama sehemu ya kuipongeza Tanzania kwa kutimiza miaka 50 ya uhuru na kuendeleza ushirikiano baina ya miji dada (sister cities) ya Milwaukee nchini Marekani na Morogoro nchini Tanzania.
Katika hafla hiyo fupi iliyohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, Meya Barrett na Balozi Maaajar walikubaliana kuendeleaza ushirikiano baina ya miji hii miwili, ulioanzishwa mwaka 2006, na pia kushawishi wawekezaji na wafanya biashara wa ukanda huu wa Marekani kuwekeza Tanzania.
Balozi Maajar yuko Jimboni Wisconsin kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu iliyoandaliwa na muasisi wa ushirikiano wa miji ya Milwaukee na Morogoro Bw. Ryan Skyfe, ambapo anakutana na taasisi za elimu, biashara na wawekezaji mbalimbali kwa nia ya kuangalia maeneo ya ushirikiano wenye tija ili kuleta maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.
Baadhi ya taasisi alizofanya nao mazungumzo ni Milwaukee Area Technical College walioko kwenye Jimbo la Wisconsin mjini Milwaukee ambao wamekubali kushirikiana na mojawapo ya chuo cha Tanzania na kutoa elimu inayolingana na mitaala ya chuo hicho ambacho kinaongoza kwenye Jimbo hili kwa kutoa elimu ya vitendo kwenye sekta ya nishati ya umeme inayowasaidia Wamerekani kupata ajira.
Wengine ni Phoenix Financial & Investment Services walioko Jimbo la Illinois mjini Chicago na Helios Solar Works walioko Jimbo la Wisconsin Mjini Milwaukee. Balozi Maajar pia alipata fursa ya kutoa mada kwenye mkutano uliovutia wakuu wa biashara na wawakilishi wa makampuni wapatao thelathini kutoka kwenye Jimbo la Wisconsin wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania.
Aidha Balozi Maajar alitumia fursa hiyo kuirajamu Tanzania na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo baina ya serikali za nchi hizi mbili kwa wananchi wake kuwekeza na kuendeleza ushirikiano kwa manufaa yao.
Kila mwaka Balozi wa Tanzania nchini Marekani  huandaa ziara mahsusi kwa ajili ya maafisa wakuu wa makampuni ya  kimarekani kutalii Tanzania na kuangalia fursa za uwekezaji na biashara nchini Tanzania. Ziara hiyo ambayo inachanganya biashara na utalii (business and leisure) imekuwa mashuhuri sana miongoni mwa wafanyabiashara wa Kimarekani ambapo mwaka huu inatarajiwa kufanyika tarehe 22 Juni – 02 Julai, 2012.
Balozi Maajar kesho tarehe 21.02.2012 anatarajia kukutana na Gavana wa Jimbo la Wisconsin Mjini Madison na baadae kuendelea na ziara yake kwenye miji ya La Farge na La Crosse Jimboni Wisconsin kabla ya kurejea mjini Washington, jimbo la District of Columbia.


Mindi Kasiga,
Wisconsin, Marekani.
20.02.2012
Sunday, February 5, 2012

Friends of Tanzania Winter Party

Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bibi Lilly Munanka akizungumza
kwenye ghafla ijulikanayo kama Winter Party inayoandaliwa kila mwaka na
mojawapo ya Taasisi zinayojishughulisha na Maendeleo ya Jamii Tanzania
(Friends of Tanzania) iliyofanyika tarehe 4.02.2012 huko Virginia

Baadhi ya wanachama wa Taasisi ya Friends of Tanzania na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Kaimu Balozi kwenye hafla hiyo iliyofanyikaVirginia tarehe 4.02.2012
  Kaimu Balozi akimshukuru Mwenyekiti wa Friends of Tanzania Bibi Patricia
Kelly (kushoto)  kwa kuandaa hafla hiyo na kwa kazi ya kujitolea kwa ajili
ya kuendeleza jamii mbalimbali nchini Tanzania.

Wednesday, February 1, 2012

Calling for Nominations
EMBASSY OF TANZANIA IN WASHINGTON DC.

Calling for Nominations of Tanzanians in the Diaspora who have excelled in their careers or who have been honored for service to the community

We invite nominations for Tanzanians in the USA who have excelled in their careers or who are known to have made a significant contribution in their field or to the community. 

This includes those who have been awarded by a renowned institution for their work and those working for International organizations at a senior leadership position. 

In sending your nominations please include the following:-         

  • A short bio of the nominee detailing his/her achievements;
  • Contact details of the nominator and the nominee including email address and telephone numbers;
  • Current photograph of the nominee in high resolution;

Nominations must be submitted via email to Suleiman Saleh 
ssaleh@tanzaniaembassy-us.org or to Mindi Kasiga at  mkasiga@tanzaniaembassy-us.org not later than February 15, 2012 (Later extended to April 15)

Those who will receive highest number of nominations or have notable awards will be included in a publication celebrating 50 years of Tanzania Mainland’s Independence. 

Should you require any further clarification please contact Suleiman Saleh at +1 202.884.1089 or at +1 202.320.2927,   or Ms. Mindi Kasiga at +1 202.884.1097 or +1202.390.7196.       

EMBASSY OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
1232, 22ND ST. NW. WASHINGTON DC 20037

February 1st, 2012